LUGHA ZA KIBANTU.
Visawe
Kwamujibu
wa matinde (2012:267) visawe ni maneno yenye maana zinazokaribiana. Kwa
mfano “uchawi” na “urogi” humaanisha
kitu kimoja. Vilevile tunaweza kusema kuwa visawe ni maneno tofauti yenye maana
sawa. Ifuatayo ni mifano ya visawe kutoka katika lugha mbalimbali za kibantu:
Kingindo
Katika
lugha ya kingindo kuna Maneno mengi ambayo husimama kama visawe, kwa mfano maneno
“Anamuungu”
na “Nnongo”
yote haya humaanisha neno moja tu ambalo ni “Mungu” katika lugha ya
kiswahili.
Kimatumbi
Mfano
wa visawe katika lugha hii ni kama vile “Anamuungu” na “Mnungu” yote haya
humaanisha neno moja tu ambalo ni “Mungu” katika lugha ya Kiswahili.
Kinyaturu
Katika
lugha hii ya kinyaturu pia kuna maneno mbalimbali ambayo huwa na maana sawa
ijapokuwa yanatamkwa na kuandikwa tofauti, kwa mfano maneno kama vile “Idimu”
na “Inkhuu”
haya yote humaanisha “Nyumba” katika lugha ya Kiswahili.
Vinyume
Kwa
mujibu wa matinde (2012:264) anaeleza kuwa vinyume ni uhusiano wa kimuundo
ambapo fahiwa ya maneno hupingana. Aidha, ni neno ambalo maana yake huwa ni
kinyume cha neno linguine. Kuna aina mbalimbali za vinyume zikiwemo vinyume vya
utoano, vinyume vya vidato, vinyume vya tofauti mkabala, vinyume vya uelekeo,
vinyume vya tathmini, na vinyume vya utenduzi. Mfano wa vinyume katika lugha ya
Kiswahili ni kama vile kufa-kuishi, dada-kaka, kaskazini-kusini, nenda-rudi,
funga-fungua n.k. Ifuatayo ni mifano ya vinyume katika lugha mbalimbali za
kibantu.
Kingindo
Kama
ilivyo katika lugha nyingine za kibantu lugha ya kingindo pia ina maneno
mbalimbali ambayo ni vinyume, mfano mzuri wa maneno hayo ni Akata-Atendaliengo
yakimaanisha Mvivu-Mchapakazi katika Kiswahili, pia maneno kama vile Aganja-Abya
ambayo humaanisha Rafiki-Adui katika lugha ya Kiswahili.
Kimatumbi
Maneno
ambayo husimama kama vinyume katika lugha ya kimatumbi ni kama vile Mkataa-Mpangakachi
ambayo humaanisha Mvivu-Mchapakazi katika lugha ya Kiswahili, pia maneno kama
vile mbwiga-abya
humaanisha Rafiki-Adui katika lugha ya Kiswahili.
Kihehe
Katika
lugha ya kihehe kuna maneno mengi sana ambao ni vinyume, maneno yafuatayo
yanabainisha dhahiri dhana hii na vinyume: Kukita-Kuwuka ambayo humaanisha Kwenda-Kurudi
katika lugha yetu ya Kiswahili, pia maneno kama vile Mhinza-Mkwamidzi ambayo
humaanisha Msichana-Mvulana katika lugha ya Kiswahili husimama kama
vinyume.
Kutokana
na mifano iliyobainishwa hapo juu tunabaini kuwa tofauti kuu kati ya visawe na
vinyume ni kwamba visawe ni maneno tofauti tofauti ambayo huwa na maana sawa
ilihali vinyume ni maneno ambayo hutamkwa na kuandikwa tofauti na hutoa maana
zinazokinzana.
Umeronimia
Kwa
mujibu wa matinde (2012:267) meronimia ni dhana inayotumiwa kuelekeza uhusiano
wa kitu kizima na sehemu zake au vijenzi vyake. Kwa mfano neno Mwili- amabalo
hujuisha kichwa, masikio, tumbo, miguu, mikono, pua n.k. ifuatayo ni mifano ya
maneno kutoka lugha za kibantu ambayo hubainisha dhana hii ya umeronimia:
Kichaga
Lugha
ya kichaga ina maneno mengi ambayo hubainisha dhana hii ya umeronimia, maneno
hayo ni kama vila, IKIRI- mambagha, nyikiri, mri, marha ambapo kwa Kiswahili
humaanaisha MTI- matawi, shina, mzizi, majani. Pia kuna maneno mengine kama
vile MNDIU-
marende, maoko, mro, ndeu ambayo humaanisha MWILI- miguu, mikono, kichwa, tumbo
katika lugha ya Kiswahili.
Kinyakyusa
Kwa
upande wa lugha ya kinyakusa pia haipo nyuma kwani kuna maneno mbalimbali
ambayo huweza kusimama kama umeronimia. Mfano mzuri wa maneno ya kinyakusa
ambayo husimama kama umeronimia ni kama vile INJENGE- lwighi, iluto
ambayo kwa upande wa Kiswahili humaanisha NYUMBA- mlango, dirisha.
Kinyaturu
Kinyaturu
kama ilivyo katika lugha nyingine kama vile kichaga na kinyakyusa pia lugha hii
ina maneno ambayo yanabainisha moja kwa moja dhana hii ya umeronimia. Kuna
mifano mingi sana ambayo inabainisha dhana hii ya umeronimia, mfano mzuri wa
maneno hayo ni kama vile: MWIRII- mnkono, mnghuu, itywe, ndaa
ambayo humaanisha MWILI- mkono, mguu, kichwa, tumbo katika lugha ya Kiswahili.
Pia kuna maneno mengine kama vile MNTYII- mirii, mantambi, intyina
ambayo humaanisha MTI- mizizi, matawi, shina katika lugha ya kiswahili.
Vitawe
Kwa
mujibu wa matinde (2012:262) vitawe ni muundo wenye maneno mbalimbali ambayo
yanahusiana kimaana na mara nyingi ya maneno hayo huwa imepanuka kadri ya mpito
wa wakati. Vitawe mara nyingi huwa na uhusiano kihistoria. Vilevile vitawe
huweza kufasiriwa kama ni maneno yenye maana zaidi ya moja. Kwa mfano neno paa
ambalo humaanisha enda juu, mnyama, na sehemu ya juu ya nyumba. Zifuatazo ni
lugha za kaibantu na mifano yake juu ya dhana hii ya vitawe:
Kichaga
Katika
lugha ya kichaga maneno yafuatayo yanabainisha dhana hii ya vitawe: neno “Mangi”
ambalo humaanisha “mungu” pamoja na “mwanamume”
Kinyakusa
Kwa
upande wa lugha ya kinyakyusa kuna maneno mbalimbali ambayo yanabainisha wazi
dhana hii ya viawe. Maneno yafuatayo yanabainisha moja kwa moja dhana hii ya
visawe: “Taka” ambalo humaanisha mungu pamoja na kijana wa kiume, pia neno
kama vile “Kisa” ambalo humaanisha huruma, huzuni, na upole,
vilevile kuna neno kama vile “Hobhokela” ambalo humaanisha samehe,
huruma na achilia katika lugha ya Kiswahili.
Kutokana
na ufafanuzi uliotolewa hapo juu tunabaini kuwa tofauti iliyopo baina ya
uremonimia na vitawe ni kwamba uremonimia ni neno la jumla linaloonesha
mjumuiko wa vitu vilivyokiunda kitu hicho wakati vitawe ni maneno yanayowakilisha
maana zaidi ya moja.
MAREJELEO
Matinde,
R, S. (2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia. Kwa Sekondari, Vyuo vya kati
na Vyuo vikuu. Serenget Bookshop:
Mwanza.
Wikipedia the free
encyclopedia/ visawe/ vinyume.
Kisawe Cha eupe
JibuFutaEusi
FutaMaoni haya yameondolewa na mwandishi.
FutaMaoni haya yameondolewa na mwandishi.
JibuFuta