NADHARIA
YA VIKOA VYA MAANA NA UHIPONIMIA
Maana ya nadharia
Mdee (2011) nadharia ni mpango wa mawazo uliotungwa
ili kueleza jinsi ya kufanya au kuelekeza jambo fulani.
Sengo (2009) nadharia
ni wazo kuu, fikra kuu, mwongozo mkuu wa mtu, watu, au jamii ya ya pahala fulani, wakati fulani
na kwa sababu fulani.
Nadharia ya vikoa vya maana
Dirk
(2010) anasema kuwa vikoa vya maana ni jozi za maneno yenye maana
zinazohusiana ambazo maana zake
zinategemeana na kwa pamoja zinatoa dhana ya kimuundo yenye uhalisia ndani
yake.
Kwa mujibu wa Wikipedia, kikoa cha maana ni msamiati
wa kiufundi katika taaluma ya isimu ambao unaeleza kikundi cha maneno
yanayohusiana kimaana.
Nadharia ya uhiponimia
Briton
(2000) anaeleza kuwa uhiponimia ni uhusiano wa kiwima ambapo hujumuishwa katika
fahiwa na neno jingine. Kwa mfano fahiwa ya mgomba, mahindi na maharage
zimejumuishwa katika mimea.
Matinde
(2012) hiponimu ni neno ambalo lina maana mahususi amabayo hujumuishwa katika
maana ya neno ambalo lina maana pana na uhiponimia ni uhusiano wa kifahiwa
uliopo baina ya neno lenye maana mahususi na neno linguine lenye maana
jumuishi.
Kwa mantiki hii tunabaini kuwa Tofauti kuu
kati ya nadharia ya vikoa vya maana
na uhiponimia ni kwamba vikoa vya maana hujumuisha maneno yenye
maana jumuishi wakati uhiponimia huwa na maneno yenye maana mahususi. Kwa mfano
neno mnyama ni kikoa cha maana
ambacho hujuisha simba, nyani, chui, nguruwe, pundamilia, tembo na kadhalika
wakati neno pundamilia ni hiponimu
amabayo huwa na maana mahususi yaani mnyama mwenye mistari mweupe na myeusi
katika ngozi yake
MAREJELEO
Briton
L.J. (2000). The structure of modern English. A linguistic Introillustrated Edition.
John Benjamin Publishing Company.
Dirk G,(2010). Theories of Lexical Semantics. Oxford
University Press: New York
Mdee, J, S (2010) Nadharia na historia ya
leksikografia. TUKI: Dares salaam.
Matinde,
R.S.(2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia, Kwa Sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu, Serengeti Education Publishers(T)
Ltd: Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni